Monday, September 8, 2014

KEHL AMTABIRIA MAKUBWA KAGAWA DORTMUND.

BEKI wa mahiri wa Borussia Dortmund Sebastian Kehl ana matumaini Shinji Kagawa anaweza kurejesha makali akiwa klabu hapo na suala la kuondoka Manchester United kiangazi hiki itakuwa ahueni kubwa kwa kiungo huyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Japan aliondoka Dortmund kiangazi mwaka 2012 lakini alishindwa kabisa kutamba katika msimu miwili aliyokuwepo Old Traffoprd na sasa amerejea tena Bungesliga baada ya kuondolewa katika mipango ya meneja mpya wa United Louis van Gaal. Kehl alikarirriwa akidai kuwa katika wiki chache za mwisho mambo hayakuwa vyema kwa Kagawa hivyo kuondoka kwake United kutamfanya atue mzigo mzito aliokuwa amebeba. Beki huyo aliendelea kudai kuwa anadhani sasa Kagawa anaweza kutulia na kurejesha makali yake kwakuwa atakuwa akicheza bila shinikizo. Kagawa amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Bundesliga na moja la DFB Pokal wakati alipokuwa Dortmund mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment