MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amesema uamuzi wa Franck Ribery kustaafu soka la kimataifa uko ndani ya sheria za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Rummenigge amesema Ribery amejadiliana na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa kuhusiana na mipango yake na wamekubaliana. Mwishoni mwa wiki iliyopita rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini alikaririwa katika mahojiano akidai kuwa Ribery anaweza kufungiwa kucheza mechi tatu katika klabu yake kwa kuamua kutoitumikia nchi yake. Lakini Rummenigge amefafanua jambo hilo kwa kudai kuwa kila kitu kimekwenda kwa mujibu wa taratibu za FIFA kwani Robery tayari amezungumza na Deschamps na hatamwita tena katika kikosi cha timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment