Monday, September 8, 2014

MAICON ATIMULIWA KAMBI YA BRAZIL KWA UTOVU WA NIDHAMU.

BEKI wa zamani wa klabu ya Manchester City, Maicon ametimuliwa katika kambi ya timu ya taifa ya Brazil kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu. Brazil ambao nio mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia kwasasa wanajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Eciador utakaochezwa kesho jijini New York, Marekani. Lakini beki huyo wa kulia anayecheza katika klabu ya AS Roma ambaye amecheza mechi 76 akiwa na Brazil hatakuwepo katika kikosi cha Dunga katika mchezo huo ambao utakuwa wa pili akiwa kocha. Maicon mwenye umri wa miaka 33 alicheza dakika zote katika mchezo wa kwanza chini ya Dunga ambapo Brazil iliitungua bao 1-0 Colombia huko Miami Jumamosi iliyopita. Beki huyo alijiunga na City akitokea Inter Miulan Agosti mwaka 2012 kwa kitita cha paundi milioni tatu lakini alishindwa kung’ara katika msimu mmoja alioitumikia klabu hiyo hatua iliyomfanya kutimkia Roma kiangazi mwaka jana.

No comments:

Post a Comment