Thursday, September 4, 2014

MARTINO AMMWAGIA SIFA DI MARIA BAADA YA KULIPA KISASI KWA UJERUMANI.

MENEJA wa timu ya taifa ya Argentina, Gerardo Martino amemmwagia sifa Andel Di Maria kuwa mmoja wa wachezaji watano bora duniani baada ya winga huyo kuwasambaratisha Ujerumani jana usiku. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ameonyesha kwa nini Manchester United wameilipa Real Madrid kitita ccha euro milioni 84 kumleta Old Trafford wiki iliyopita kwa kufunga bao moja huku akitengeneza mengine matatu yaliyofungwa na Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez katika ushindi wa mabao 4-2 waliopata dhidi ya mabingwa hao wa dunia. Andre Schurrle na Mario Gotze waliifungia Ujerumani mabao wawili ya kufuta machozi lakini usiku wa jana ulikuwa wa kipekee kwa Di Maria ambaye alionyesha kiwango cha hali ya juu. Akihojiwa mara ya baada ya mchezo huo Martino ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona alikipongeza kikosi chake hususani Di Maria kwa kuonyesha ubora wake. Katika mchezo huo Martino alilazimika kutowatumia nyota wake wengine kama Gonzalo Higuaini na Lionel Messi ambao ni majeruhi.

No comments:

Post a Comment