KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink amedai kuna nafasi ndogo sana kwa winga Arjen Robben kuwepo katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Czech Jumanne ijayo. Akihojiwa kabla ya mchezo wao wa kirafiki dhidi dhidi ya Italia baadae leo, Hiddink amesema kwa inavyoonekana itakuwa ngumu kwa mchezaji huyo kucheza mchezo wa Jumanne kwasababu bado hawana mawasiliano naye. Robben kwasasa anajiuguza majeraha ya kifundo cha mguu ambao ndio yanamfanya kuukosa mchezo huo wa leo lakini nyota huyo anadhani anaweza kupona kwa wakati kabla ya mchezo huo wa kufuzu. Hata hivyo Hidink ameonya itakuwa ngumu kwa mchezaji huyo kufanya mazoezi kwa kipindi kifupi kabla ya mchezo huo kwasababu hajafanya mazoezi yoyote mpaka hivi sasa.
No comments:
Post a Comment