Friday, September 12, 2014

CHELSEA WAMPA COURTOIS MKATABA MPYA.

KLABU ya Chelsea ambao ndio vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza wametangaza jana kumpatia mkataba mpya wa miaka mitano golikipa wa kimataifa wa ubelgiji Thibaut Courtois. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 22 alirejea Stamford Bridge msimu huu baada ya kucheza kwa mkopo wa miaka mitatu katika klabu ya Atletico Madrid na sasa anaonekana kuchukua nafasi ya Petr Cech kama chaguo namba moja la meneja Jose Mourinho. Courtois aliuambia mtandao wa Chelsea kuwa amefurahishwa kusaini mkataba huo mrefu na sasa anataka kutilia mkazo kazi yake ili aweze kuisaidia timu hiyo kufika mbali. Courtois alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Genk ya Ubelgiji mwaka 2011 lakini haraka alipelekwa kwa mkopo Atletico ambako alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu na kutinga fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Golikipa huyo pia amecheza mechi za kimataifa 23 huku akiwemo katika kikosi cha timu ya taifa cha Ubelgiji kilichotinga robo fainali ya michuano ya Kombe Dunia nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment