WANANDOA wawili nchini Argentina wameshinda kesi kupinga sheria kali inayohusu majina ya watoto na kutoa heshima kwa shujaa wao katika soka kwa kumpa jina la Messi motto wao aliyezaliwa. Baba wa mtoto huyo Daniel Varela alikuwa na ndoto za muda mrefu kumpa jina la nyota huyo baada ya kumuona kwa mara ya kwanza akiitumikia timu ya taifa ya vijana ya Argentina. Baada ya kupata watoto wawili wa kike na kusubiri kwa miaka mingine nane, Varela hakutaka sheria zilizopo zimzuie kutimiza ndoto yake hiyo. Varela alituma maombi katika mamlaka husika kupewa ruhusa ya kutumia jina hilo ambapo kwa shertia za huko hairuhusiwi watoto kupewa majina ya pili. Akielezea furaha yake baada ya kufanikiwa ombi lake, Varela mwenye umri wa miaka 35 amesema alimuona Messi wakati akiwa na umri wa miaka 17 na baadae aligundua kuwa mchezaji huyo ni mnyenyekevu, mtu mzuri ndio maana akawaza kumpa mwanae wa kiume jina hilo.
No comments:
Post a Comment