MSHAMBULIAJI nyota wa Juventus, Carlos Tevez amebainisha kuwa tetesi kuwa hayuko fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Udinese kesho sio za kweli. Taarifa kutoka katika vyombo vya habari vya Italia zimedai kuwa kocha Massimiliano Allegri atakuwa bila nyota wake huyo katika mchezo wa kwanza wa nyumbani toka ateuliwe kushika nafasi hiyo. Hata hivyo, Tevez ambaye ameendelea kukosekana katika kikosi cha timu ya taifa baada ya kocha mpya kumuacha wakati akitangaza kikosi chake cha kwanza mwezi huu, alipuuza taarifa hizo na kudai kuwa yuko fiti. Tevez aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter, akiwashukuru wale wote wanaomjali lakini aliwahakikishia kuwa yuko fiti na hana majeruhi yoyote. Tevez amefunga mabao 21 akiwa na Juventus msimu uliopita akielewana vyema na mshambuliaji mwenzake Fernando Llorente ambaye naye alifunga mabao 18.
No comments:
Post a Comment