MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Alexandre Lacazette amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Lyon ambao utamuweka hapo mpaka msimu wa 2017-2018. Lacazette ambaye amekuwa akipikwa na mabingwa wa zamani wa Ufaransa toka akiwa na umri wa miaka 10, amefunga mabao 42 katika mechi 154 alizoichezea timu hiyo toka aibuke katika kikosi cha kwanza. Msimu ulioppita mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao 15 lakini ahakuitwa katika kikosi cha timu ya taifa kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Lacazette ambaye ameichezea Ufaransa mechi tatu alikuwepo katika kikosi cha nchi hiyo kilichotoa sare ya bao 1-1 na Serbia wiki iliyopita katika mchezo wa kirafiki akiziba nafasi ya Olivier Giroud.
No comments:
Post a Comment