MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema mshambuliaji Danny Welbeck aliachwa kwasababu hakufunga mabao ya kutosha huku akidai kuwa atawapa nafasi wachezaji ndani. Akiongeza wakati wa kuwatambulisha wachezaji wawili waliosajili mwishoni Radamel Falcao na Daley Blind, Van Gaal alifafanua kwanini Welbeck mwenye umri wa miaka 23 aliuzwa katika klabu ya arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16. Van Gaal amesema Welbeck amecheza misimu mitatu akiwa na kikosi cha kwanza lakini hajafikia rekodi ya Robin van Persie au Wayne Rooney katika ufungaji. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa hiyo ndio sababu iliyomfanya auzwe kwasababu ya Falcao na pia kutoa nafasi kwa wachezaji chipukizi nao kupata nafasi.
No comments:
Post a Comment