SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast limedai kuwa beki Serge Aurier anayecheza klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ambaye alizimia baada ya kugongana vichwa katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Cameroon aanaendelea vyema. Shirikisho hilo nlimedai kuwa tukio hilo lilikuwa la kuogofya lakini wanashukuru hakuna tatizo lolote kubwa lililotokea kwa mchezaji huyo. Hata hivyo klabu ya PSG imedai kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 21 atafanyiwa vipimo zaidi ili kujiridhisha na afya yake kabla ya kuruhusiwa kucheza tena. Katika mchezo huo uliochezwa jijini Younde, Ivory Coast walipata kipigo kikali cha mabao 4-1 na kushuhudia Aurier akigongana na kuzimia na mshambuliaji wa Cameroon Kweuke Leonard katika dakika ya 55 ya mchezo. Katika taarifa yake shirikisho hilo limedai kuwa matitabu aliyopatiwa baada ya kuzimia na madaktari wa timu hiyo yalitosha kumfanya azinduke na kuweza kukaa katika benchi la wachezaji wa akiba kufuatilia dakika zilizobakia za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment