MCHEZAJI mmoja amevamiwa na kundi la wahuni na kuvuliwa fulana na kaptura yake wakati wa mchezo wa ligi za chini nchini Argentina. Gazeti moja nchini humo lilinasa picha za video za tukio hilo ambapo Elias Di Biasi kiungo wa timu ya Deportivo Italiano inayoshiriki ligi daraja la nne akivuliwa nguo zake na kubakiwa amesimama na nguo ya ndani. Mchezaji huyo amesema mwanzoni alijaribu kupambana nao lakini walikuwa wako watatu hivyo walimzidi nguvu. Tukio hilo lilitokea Juzi katika dakika ya 60 ya mchezo dhidi ya Villa San Carlos ambao ulishuhudia Deportivo wakifungwa mabao 3-0. Kundi la wahuni kadhaa wakiwa wamevalia makoti yaliyofunika nyuso zao walivamia uwanjani kufanya tuio hilo na kisha kurejea jukwaani. Di Biasi alipewa jezi nyingine ili aweze kuendelea na mchezo ambao ulisimamishwa kwa dakika kadhaa.
No comments:
Post a Comment