SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA linajipanga kumtangaza Milovan Rajevac kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Black Stars kwa mkataba wa miaka miwili. Kocha anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kwesi Appiah baada ya taarifa kudai kuwa Mserbia huyo alifaulu mahoajiano jana baada ya kuwepo nchini humo kwa muda wa siku tatu. Appiah alifanya kazi na kocha huyo kati ya mwaka 2009 mpaka alipoondoka baada ya michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2010. Inaaminika kuwa kocha huyo ndio aliyekisuka kikosi cha Ghana kilichofanya vyema katika michuano hiyo ya Afrika Kusini na GFA wameona huo ndio utakaokuwa muwa arobaini wa timu hiyo ili kuirejeshea makali yake ambayo yanaonekana kupotea chini Appiah. Ghana kwasasa wanafukuzia nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani baada ya kuitandika Togo mabao 3-2 Juzi na kuchupa mpaka nafasi ya pili katika kundi E nyuma ya Uganda.
No comments:
Post a Comment