Friday, September 12, 2014

PISTORIUS AKUTWA NA HATIA YA KUMUUA MPENZI WAKE BILA HATIA.

MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya. Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipa alimema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake. Masipa aliendelea kudai kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp kwa kutekeleza mauaji hayo kwa makusudi. Mwanariadha huyo pia amepatikana na hatia ya kosa la kutumia sialaha yake isivyopaswa katika mgahawa mmoja jijini Johannesburg.

No comments:

Post a Comment