KOCHA wa timu ya taifaya Ureno, Paulo Bento amepoteza kibarua chake jana baada ya kuanza vibaya kampeni za kufuzu michuano ya Ulaya. Shirikisho la Soka la Ureno, lilithibitisha kuondoka kwa kocha huyo hatua ambayo ilitazamamiwa kufuatia kufungwa bao 1-0 nyumbani na Albania Jumapili iliyopita. Mashabiki wa Ureno waliizomea timu yao baada ya kipigo hicho cha Albania na kumuongezea shinikizo kocha huyo ambaye alikiri baada ya mchezo huo kuwa kikosi chake kilicheza chini ya kiwango. Baada ya kufanya kazi kwa mafanikio katika klabu ya Sporting Lisbon ambapo aliisaidia timu hiyto kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara nne mfululizo, Bento alichukua mikoba ya kuinoa Ureno kutoka Carlos Quiroz mwaka 2010. Ureno ikiwa chini yake ilifanikiwa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2012 kupitia hatua ya mtoano lakini waliondolewa katika michuano hiyo na aliyekuja kuwa bingwa Hispania katika hatrua ya nusu fainali. Bento alifanikiwa kuiwezesha Ureno kufuzu Kombe la Dunia nchini Brazil kwa kupitia hatua ya mtoano tena lakini safari hii alishindwa kufurukuta na kujitoka waking’olewa katika hatua ya makundi. Ureno inakabiliwa na mchezo mwingine wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Denmark Octoba 14 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment