MABINGWA wa soka barani Afrika, Nigeria inaonekana wameepuka kufungiwa mechi za kimataifa baada ya msuguano wa uongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo kumalizika. Hatua hiyo imekuja kufuatia Chris Giwa kuamua kunyoosha mikono na kuacha kung’ang’ania madaraka ya urais wa shirikisho hilo katika siku ya muda wa mwisho uliotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Wiki iliyopita FIFA iliipa nchi hiyo mpaka Jumatatu Giwa awe ameachia madaraka na kama hilo lingeshindakana wangefungiwa kushiriki mechi za kimataifa. Kama Nigeria ingefungiwa moja kwa moja wangekuwa wameukosa mchezo wa kufuzu Mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini. Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi leo katibu mkuu ambaye ndiye anayetambulika na FIFA Musa Amadu amesema kilikuwa ni kipindi kigumu katoka soka la nchi hiypo lakini anashukuru suala hilo sasa limepita. Kwa matokeo hayo sasa inamaanisha kuwa bodi ya NFF ikiwa chini ya rais Aminu Maigari inaweza kuanza mikakati ya uchaguzi ambao unatakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment