KIUNGO mpya wa Chelsea, Cesc Fabregas amekiri kuwa wazo la kuitumikia klabu hiyo chini ya Jose Mourinho lilikuwa ni wazo lisilofikirika kwake katika kipindi cha nyuma. Nyota huyo wa zamani wa Arsenal, alirejea Ligi Kuu katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya kushindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Barcelona. Fabregas amesema kama mtu angemuambia miaka mitano nyuma kwamba atakwenda kucheza Chelsea chini Mourinho ni jambo abalo asingeamini lakini maisha yanabadilika. Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa alianza kufikiria kuondoka Barcelona baada ya fainali ya Kombe la Mfalme ambayo walifungwa na Real Madrid ambapo baada ya kuzungumza na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta aliona kama amewapunguzia bugudha kutokana na kauli yake. Baada ya hapo alimuomba wakala wake amtafutie timu nyingine na Chelsea wakatoa ofa ambapo baada ya kuzungumza na Mourinho na kumwambia mambo anayohitaji akaona hapo ndio patakapomfaa.
No comments:
Post a Comment