Monday, September 8, 2014

SASA MAKOCHA KUPEWA NAFASI YA KUWAKOSOA WAAMUZI.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ametangaza kuwa makocha sasa wanaweza kuhoji maamuzi ya waamuzi kwa kuanzisha utaratibu mpya wa kusikiliza kesi za makosa ya waamuzi kwa kutumia ushahidi wa picha za video. Blatter mwenye umri wa miaka 78 amesema anataka makocha waruhusiwe kuhoji uamuzi wa mwamuzi mara moja kwa kila nusu ya mchezo. Rais huyo ambaye pia amethibitisha nia yake ya kugombea kipindi kingine, aliendelea kudai kuwa makocha watakuwa na haki ya kuhoji maamuzi ya mwamuzi mara mbili au moja lakini wakati mchezo utakapokuwa umesimama. Masema baada ya hapo mwamuzi na kocha watakwenda kuangalia kipande cha sehemu makosa yalipofanyika na baadae mwamuzi anaweza kubadili uamuzi wake kama ilivyo katika mchezo wa tenisi. Blatter amesema utaratibu huo mpya unaweza kuanza kutumika mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment