KLABU ya Borussia Dortmund imethibitisha kuwa Marco Reus anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Scotland jana. Mshambuliaji alikosa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kutokan ana majeruhi ya kifundo cha mguu aliyopata mwishoni mwa msimu uliopita na sasa inaonekana tatizo limejirudia kwa kujitonesha. Hata hivyo Dortmund katika taarifa yake wamedai kuwa majeruhi hayo aliyopata Reus mwenye umri wa miaka 25 sio makubwa sana kama yale yaliyopita. Reus sasa anakabiliwa na changamoto ya kuwa fiti kwa ajili mechi za kufuzu za Ujerumani zinazofuata ambazo zitakuwa dhidi ya Poland na Jamhuri ya Ireland katikati ya Octoba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment