Tuesday, September 9, 2014

MASHABIKI WAMEPOTEZA IMANI NA TIMU YAO - OWEN.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Michael Owen amedai kuamini kuwa nchi hiyo imepoteza imani na timu yao ya taifa. Akizungumza katika mkutano wa Soccerex jijini Manchester, mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool amesema kushindwa kwao kufanya vyema katika michuano mikubwa ndio jambo lililochangia suala hilo. Owen mwenye umri wa miaka 34 amesema kila mtu wakiwemo na mashabiki wamepoteza imani yao kwa timu ya taifa na hadhani kama inaweza kurejea mpaka wafanye jambo katika michuano mikubwa. Nyota huyo amesema kuwa wakati matokeo ya ushindi dhidi ya Switzerland jana katika michuano ya kufuzu michuano ya Ulaya yakiwa yanatia moyo lakini hadhani kama ushindi katika mechi utasaidia sana. Kwa kipindi kirefu nchi hiyo imekuwa ikipata matokeo yasiyo yakuridhisha hivyo ni muhimu kuendelea kufanya vyema zaidi katika michuano inayokuja ilo kurejesha imani.

No comments:

Post a Comment