Tuesday, September 9, 2014

RAIS MPYA WA SOKA ITALIA APANIA KUWAHENYESHA WACHEZAJI WAGENI.

RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Italia-FIGC, Carlo Tavecchio amebainisha kuwa anataka kuungwa mkono na serikali ili kupunguza idadi ya wachezaji walioko nje ya muungano wa Ulaya nchini humo. Rais huyo mwenye umri wa miaka 71 alichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi ulioleta utata kutokana na kauli yake kuhusu wachezaji weusi iliyotafsiriwa kama ni kibaguzi. Sasa Tavecchio amebainisha kuwa anataka kuleta sheria itakayowalazimisha vilabu vikubwa kuchezesha walau wachezaji wanne wa Italia katika kila mchezo huku akitaka idadi hiyo kupanda na kufikia sita ifikapo msimu wa mwaka 2015-2016. Kiongozi huyo pia anataka kuweka idadi ya wachezaji 25, nane kati yao wawe wametoka katika timu za vijana na kuweka sheria kali kwa wachezaji walioko nje ya Umoja wa Ulaya kupewa kibali cha kucheza soka Italia. Tavecchio amesema hatu hiyo itasaidia kulinda vipaji vya vya soka vilivyopo nchini humo ambavyo kwa siku za karibuni vimeonekana adimu kutokana na kukosa kupewa nafasi kutokana na wingi wa wachezaji wa kigeni.

No comments:

Post a Comment