KIUNGO wa kimataifa wa Uholanzi Wesley Sneijder anafiriki hakutendewa vyema na Inter Milan lakini bado ana matumaini klabu hiyo itashinda taji la Ligi Kuu msimu huu. Sneijder alikuwa mmoja wa nyota wa kikosi cha Inter waliofanikiwa kunyakuwa mataji matatu katika msimu wa 2009-2010, lakini baadae aliachwa baada ya kukataa kukubalia kukatwa mshahara wake. Nyota huyo aliondoka na kuhamia katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki Januari mwaka 2013 ingawa bado hasahau jinsi wajumbe ya bodi wa timu hiyo walivyomfanyia. Akihojiwa Sneijder amesema pamoja na kufanyiwa vitendo visivyo vya uungwana na viongozi wa klabu hiyo lakini bado anaipenda Inter na anawaombea kufanya vyema kwa ajili ya mashabiki wao. Sneilder amesema kwa kipindi kirefu vilabu kutoka Milan vimekuwa havifanyi vyema kama mashabiki wao walivyozoea kitendo ambacho kimetoa nafasi kwa Juventus kutamba huku Roma nao wakija kwa kasi. Kiungo huyo mchezeshaji kwasasa ana mkataba na Galatasaray unaomalizika Juni mwakani.
No comments:
Post a Comment