Sunday, October 5, 2014

BUFFON AMTETEA MWAMUZI BAADA YA KUICHAPA ROMA.

NAHODHA wa klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon amemkingia kifua mwamuzi Gianluca Rocchi baada ya ushindi wa mabao 3-2 waliopata dhidi ya mahasimu wao AS Roma. Katika mchezo huo uliozua utata mwamuzi huyo aliizawadia penati mbili Juventus ambazo zote zilifungwa na Carlos Tevez wakati pia alishindwa kung’amua Arturo Vidal alikuwa ameotea katika lango la Roma na kutoa kwa Leonardo Bonucci kufunga bao la ushindi dakika za mwisho. Mara baada ya mchezo huo nahodha wa Roma Fancesco Totti alimshambulia mwamuzi huyo kwa kushindwa kuchezesha ipasavyo lakini Boffon anadhani mwamuzi hapaswi kulaumiwa. Buffon amesema huwezi kukosoa uwezo wa mwamuzi aliyekuwa na uzoefu wa kipindi kirefu kama Rocchi, na anachoamini yeye timu zote mbili zilionyesha mchezo wa kiwango cha juu. Golikipa huyo wa kimataifa wa Italia aliendelea kudai kuwa iko wazi kuwa Roma hivi sasa wako imara kuliko ilivyokuwa msimu uliopita ndio maana mchezo huo ulikuwa mgumu.

No comments:

Post a Comment