Sunday, October 5, 2014

RONALDO ANASTAHILI BALLON D'OR - ANCELOTTI.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini kuwa Cristiano Ronaldo anastahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa msimu wa 2014-2015. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno alifunga mabao matatu au hat-trick katika mechi nne za La Liga katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Athletic Bilbao na kufikisha idadi ya mabao 13 mpaka sasa. Ukiongeza pia na jinsi alivyotoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, Ancelotti ana uhakika kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 anastahili kupewa tena tuzo hiyo. Akihojiwa Ancelotti amesema anafikiri hakuna wasiwasi kuhusu Ronaldo kushinda tena tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu hususani kutokana na kiwango cha hali ya juu alichoonyesha. Kocha aliendelea kudai kuwa washambuliaji wake wote watatu walicheza vyema katika mchezo huo ambao Ronaldo na Karim Benzema walifunga huku Gareth Bale akitoa pasi za mwisho na kufanya juhudi kubwa.

No comments:

Post a Comment