MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amepuuzia mzozo wake na meneja wa Chelsea Jose Mourinho wakati kikosi chake kilipotandikwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu jana. Wawili hao walikwaruzana baada ya mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kukwatuliwa na Gary Cahill wa Chelsea katikati ya kipindi cha pili ambapo Wenger alimsukuma Mourinho kifuani. Wawili hao walitenganishwa na kamisaa wa mchezo huo Jonathan Moss ambapo ingawa Wenger anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa tukio lake hilo mwenyewe amelipa uzito mwepesi wakati akihojiwa. Wenger aliwaambia wana habari kuwa hajutii kiti alichofanya kwani haoni kosa lake kwani alizuia kwenda alipotaka bila sababu yoyote. Wenger amesema alichokuwa akitaka yeye ni kwenda kumuangalia mchezaji wake aliyeangushwa chini lakini Mourinho akamzuia ndio maana ikatokea kutoelewana baina yake lakini katika mpira jambo hilo ni la kawaida. Kwa upande wake Mourinho amesema alimzuia Wenger kwakuwa alijua anakata kumshinikiza mwamuzi kutoka kadi nyekundu kwa faulo aliyocheza Cahil.

No comments:
Post a Comment