Monday, October 20, 2014

GHANA WAKWEPA OMBI YA CAF KIAINA.

RAIS wa Ghana, John Mahama amesema nchi bado haijafanya maamuzi kama wakubalia kuwa wenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani au la. Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limeziandikia nchi kadhaa kufikiria kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kama Morocco itaamua kujitoa kutokana na mlipuko hatari wa ugonjwa wa Ebola hususani katika nchi za Afrika ya Magharibi. Waziri wa michezo wa Ghana Mahama Ayariga ameeleza kuwa nchi hiyo ambayo imewahi kunyakuwa taji la michuano hiyo mara nne ina miundo mbinu ya kutosha kuwa mwenyeji huku kukiwa kumebakiwa miezi mitatu na wanafikiria ombi hilo la CAF. Kauli yake hiyo imekosolewa vikali na Chama cha Madaktari wan chi hiyo na asasi zingine za kiraia ambao wamedai kuwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kunaifanya nchi nzima kuwa katika hatari ya kulipukiwa na ugonjwa huo ambao tayari umeshaua watu 4,500 mpaka sasa. Katika mkutano wake Mahama alipoza hofu za wananchi wa Ghana na kudai kuwa hakuna uamuzi wowote uliofikiwa mpaka sasa kuhusu kuandaa michuano hiyo inayoshirikisha nchi 16.

No comments:

Post a Comment