MENEJA wa klabu ya Swansea City, Garry Monk amesema mchezaji wa Stoke City Victor Moses anapaswa aone haya na kuadhibiwa kwa kuisaidia timu yake kupata penati. Moses alizawadiwa penati katika dakika ya 43 kwa kuangushwa na beki wa Swansea angel Rangel na kuifanya Stoke kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja Britannia. Monk ambaye timu yake imeshindwa kupata ushindi katika mechi tano za ligi amesema Moses anapaswa kuadhibiwa kwa kudanganya na kujirusha. Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa vikali na kocha wa Stoke Mark Hughes aliyedai kuwa kauli ya Monk haikubalikin kwani sio kweli kuwa mchezaji wake alijirusha.

No comments:
Post a Comment