Monday, October 20, 2014

RONALDO NA BALE WANGEWEZA KUWA MABINGWA OLIMPIKI KAMA WANGEAMUA KUWA WANARIADHA - RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers ameonyesha kuwahusudu Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuelekea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Rodgers amesema anaamini kuwa wawili hao wangepata mafanikio katika mashindano ya riadha ya olimpiki kama wangeamua kufanya kazi tofauti. Liverpool inahitaji matokeo mazuri katika mchezo wao huo wa Jumatano utakaofanyika Anfield baada ya kupata kipigo cha kushtusha katika mchezo uliopita dhidi ya FC Basel. Pamoja na hayo Rodgers ameonya kuwa haitakuwa kazi rahisi kwa timu yake kupata matokeo wanayohitaji kutokana vipaji vya mchezaji mmoja mmoja walivyo navyo Madrid. Rodgers amesema Madrid wana vipaji vya hali ya juu na jinsi wanavyocheza inawafanya kuwa timu hatari kukutana nayo. Madrid kwasasa ndio wanaoongoza kundi B wakiwa na alama sita kutokana na michezo miwili waliyocheza Liverpool wako nafasi ya pili wakikabana koo na Basel wote wakiwa na alama tatu.

No comments:

Post a Comment