Thursday, October 16, 2014

KESHI ATIMULIWA NIGERIA.

SHIRIKISHO la Soka la Nigeria-NFF, limeamua kumtimua rasmi kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Steven Keshi pamoja na ushindi waliopata nyumbani dhidi ya Sudan na kufufua matumaini yao ya kutetea taji lao la michuano Mataifa ya Afrika mwakani. Katika taarifa yake NFF imedai kuwa ilifikia uamuzi wake huo leo katika kikao chao cha dharura walichokutana na kocha wa zamani Shuaibu Amodu ndio atakayechukua nafasi ya kama kocha wa muda mpaka atakapoteuliwa kocha mpya wa kigeni. Nigeria walikuwa wakiburuza mkia katika kundi A baada ya kuambulia alama moja katika mechi zao tatu za kufuzu AFCON lakini ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Sudan jijini Abuja jana umewapandisha mpaka nafasi ya tatu katika msimamo. Tetesi za mustakabali wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 zilikuwa zikivuma toka baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo Nigeria ilitinga hatua ya timu 16 bora. Mkataba wa miaka mitatu wa Keshi kuinoa Super Eagles ulimalizika baada ya Kombe la Dunia lakini aliambiwa aendelee kuinoa timu hiyo kwa mkataba maalumu wa muda wa suala lake likishughulikiwa.

No comments:

Post a Comment