Thursday, October 16, 2014

MESSI ATETEWA NA BABA YAKE KESI KUKWEPA KODI.

BABA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa mwanae huyo hahusiki na masuala yake ya kodi na hivyo hapaswi kujumuishwa katika uchunguzi wa tuhuma za ukwepaji kodi. Messi na baba yake Jorge ambao walikana tuhuma hizo wanatuhumiwa na Mamlaka ya Hispania kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha euro milioni nne kati ya mwaka 2007 mpaka 2009. Hatua hiyo imekuja kufuatia madai kuwa mapato ya Messi katika haki za kutumia picha zake zilifichwa kwa kutumia makampuni kutoka Uruguay, Belize, Switzerland na Uingereza. Jorge amesema mara zote amekuwa akisisitiza kuwa mwanae hahusiki na suala hilo kwani ni jambo linalomhusu yeye na wakili wake analishughulikia. Messi amekuwa mkazi wa jiji la Barcelona toka mwaka 2000 na alipata uraia rasmi mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment