Sunday, October 5, 2014

LANGALANGA: BIANCHI KUFANYIWA UPASUAJI BAADA YA KUPATA AJALI YA MASHINDANI YA JAPAN GRAND PRIX.

DEREVA wa langalanga kutoka timu ya Marussia Jule Bianchi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya majeraha kadhaa kichwani katika michuano ya Grand Prix ya Japan. Mapema, Shirikisho la Kimataifa la Langalanga-FIA lilidai kuwa dereva huyo Mfaransa atafanyiwa upasuaji kabla ya kuhamishiwa chumba cah wagonjwa wenye uangalizi maalumu. Bianchi mwenye umri wa miaka 25 alikuwa hajitambui wakati akipelekwa hospitalini akitokea Suzuka kulikofanyika mashindano hayo. Dereva huyo aliumia wakati alipogonga gari lililokuwa likitolewa barabarani katika mzunguko wa 44 wa mashindano hayo ambayo yaliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua iliyokuwa ikinyesha muda wote.

No comments:

Post a Comment