Wednesday, October 8, 2014

MOSES KUKAA NJE UWANJA WIKI TATU.

WINGA majeruhi wa kimataifa wa Nigeria, Victor Moses anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu. Moses alipata majeruhi hayo katika mchezo wa Ligi Kuu ambao klabu yake ya Stoke City ilichabangwa kwa mabao 3-1 na Sungerland Jumamosi iliyopita. Nyota huyo sasa atabakia katika klabu yake kwa ajili ya matibabu huku akitarajiwa kurejea katika kikosi cha kwanza cha Stoke baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. Meneja wa Stoke Mark Hughes amesema Moses atafanyiwa tena upasuaji kuangalia ukubwa wa tatizo la msuli linalomsumbua lakini anategemea halitakuwa tatizo kubwa.

No comments:

Post a Comment