MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amempongeza Karim Benzema kama mshambuliaji bora katika La Liga baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo walioitandika Athletico mabao 5-0 jana. Benzema amekuwa akizomewa na mashabiki wa nyumbani msimu huu lakini jana jina lake lilikuwa likiimbwa kwa kutukuzwa katika uwanja wote wa Santiago Bernabeu. Pamoja na Ronaldo kupiga hat-trick katika mchezo huo lakini hakushindwa kumpongeza mchezaji mwenzake huyo kwa kurejesha imani kwa mashabiki wa timu hiyo. Ronaldo amesema kukosolewa ni sehemu ya mchezo wa soka, hivyo anafurahi kuwa sasa Benzema hana ugomvi tena na mashabiki kwani amewapa wanachokitaka. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa amekuwa akifurahia sana muungano wake na Benzema pamoja na Gareth Bale katika timu hiyo.

No comments:
Post a Comment