WINGA wa zamani wa klabu za Arsenal na West Ham United, Freddie Ljungberg amesema Ligi Kuu mpya iliyoanzishwa nchini India itakuwa na mafanikio. Ljungberg mwenye umri wa miaka 37 anatarajiwa kucheza sambamba na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea Nicolas Anelka mwenye umi wa miaka 35 katika timu ya Mumbai City inayonolewa na meneja wa zamani wa Sunderland Peter Reid. Akihojiwa Ljungberg ambaye amewahi kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Arsenal amesema katika mchezo wao kwanza wanatarajiwa kuwepo mashabiki wapatao 110,000 hivyo hiyo ni dalili nzuri ya kuonyesha mafanikio katika ligi hiyo. Ligi Kuu nchini India inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba 12 mwaka huu na itadumu ka kipindi cha wiki 10. Nyota waliowahi kushinda Kombe la Dunia akiwemo Alessandro Del Piero, Marco Materazzi, David Trezeguet na Robert Pires ni miongozi mwa wachezaji wenye majina makubwa watakaocheza katika ligi hiyo kwa madhumuni ya kuiongezea umaarufu.

No comments:
Post a Comment