MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anadhani baadhi ya maamuzi yalikwenda kinyume kwa timu kwa timu yake wakati Manchester United walipofanikiwa kusawazisha katika mwisho na kupata sare katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Old Trafford. Chelsea walianza kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Didier Drogba kabla ya Robin van Persie hajasawazisha katika dakika za majeruhi baada ya Branislav Ivanovic kutolewa kwa kadi nyekundu. Akihojiwa Mourinho amesema aliona kadi hiyo ikimnyemelea beki wake huo lakini akaongeza kuwa kama atataka kuongelea kuhusu hilo lazima azungumzie penati ya Ivanovic ambayo hakupewa. Chelsea sasa inakabiliwa na adhabu ya faini ya paundi 25,000 kwa wachezaji wake kupata kadi za njano zaidi ya sita katika mchezo mmoja. United wao walishawahi kuadhibiwa kwa kosa kama hilo mwaka 2008 kwa kupata kadi za njano saba katika mchezo baina ya timu hizo katika Uwanja wa Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment