MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amemlaumu kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Vicente del Bosque kutokana matatizo ya majeruhi ya Diego Costa. Mourinho amesema majeruhi ya msuli kwa Costa yalitokana na kuchezwa mechi mbili katika muda wa siku tatu wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa yeye mwenyewe alikuwa akimtumia Costa kwa tahadhari lakini hali haikuwa hivyo wakati alipokuwa na Hispania. Akiulizwa kama anadhani Costa tatizo la Costa limekwisha, Mourinho alikubali lakini akadai kuwa nyota huyo bado atahitajika kuitumikia tena nchi yake Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment