Monday, October 20, 2014

MULLER AIGWAYA ROMA.

KIUNGO wa kimataifa wa Ujerumani, Thomas Muller anategemea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Roma utakuwa mkali wakati Bayern Munich itakaposafiri kuifuata timu hiyo ya zamani ya Pep Guardiola. Akihojiwa mara baada ya mazoezi jana kuelekea katika mchezo wao huo wa kundi E huko Rome, Muller amesema hategemei matokeo kupatikana mapema huku akiamini kila timu ina nafasi sawa ya kuondoka na alama zote tatu. Muller jambo la muhimu watalofanya ni kuhakikisha wanaondoka hata na alama moja ili waweze kuendelea kuongoza kundi hilo. Kama Bayern wakifanikiwa kushinda mechi zao mbili zinazofuata wanatakuwa wamejihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano katika michuano hiyo. Guardiola aliwahi kuichezea Roma mechi nne za Serie A na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu wa 2002-2003 wakati akikaribia kutundika daruga zake.

No comments:

Post a Comment