Monday, October 20, 2014

VAN GAAL AWAPASHA WANAOMKOSOA.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema ni upuuzi kuwaambia wamtathmini katika miezi mitatu ya kwanza Old Trafford. Wakati Mholanzi huyo anachukua mikoba ya kuinoa timu hiyo Julai mwaka huu alidai kuwa mbinu zake zitaanza kuzaa matunda baada ya miezi mitatu. Baada ya muda huo kumalizika United sasa wako katika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kupoteza michezo miwili. Akihojiwa Van Gaal mwenye umri wa miaka 63 amesema ilikuwa ni upuuzi kusema miezi mitatu kwasababu vyombo vya habari vimekuwa vikizungumzia muda huo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa siku zote amekuwa akiangalia kiwango lakini mara zote huwa kinaweza kushuka au kupanda kutegemeana na mchezo. Kama wakishinda mchezo wao wa leo dhidi ya West Bromwich Albion, United watakuwa wameshinda mechi ya tatu mfululizo katika ligi kwa mara ya kwanza toka mwaka huu uanze.

No comments:

Post a Comment