Tuesday, November 4, 2014

BARTOMEU AKANUSHA BARCELONA KUWA KATIKA MGOGORO.

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wowote Camp Nou na kudaio kocha Luis Enrique bado anaungwa mkono na klabu hiyo. Baada ya kuanza vyema msimu wa La Liga, Barcelona walijikuta wakiteleza kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya nne katika msimamo wa ligi kufuatia vipigo viwili mfululizo dhidi ya Real Madrid na Celta Vigo. Kumekuwa na taarifa kutoka vyombo vya habari vya Hispania kuwa wachezaji nyota wa timu hiyo hawakufurahishwa na kikosi kilichoanza na mbinu walizoelekezwa wakati walipofungwa na mabao 3-1 na Madrid. Hata hivyo, Bartomeu amesema haamini kama kufungwa mechi mbili kutaleta tatizo lolote kwani bado wana imani kuwa Enrique ndiye mtu sahihi kwa kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment