HATIMAYE Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, limeiteua Equatorial Guinea moja nchi ndogo kabisa barani Afrika kuchukua nafasi ya Morocco kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwakani. Morocco walikuwa wanataka michuano hiyo kuahirishwa kutokana na wasiwasi wa kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Ebola lakini CAF ilikataa ombi hiyo Jumanne iliyopita na kuivua uenyeji taifa hilo lililopo kaskazini mwa bara hili. Eguatorial Guinea ambao wana utajiri wa mafuta walikuwa wenyeji wa michuano ya Afcon mwaka 2012 wakiwa sambamba na majirani zao Gabon lakini sasa wataandaa michuano hiyo inayoshirikisha nchi 16 wao wenyewe kuanzia Januari 17 hadi Februari 8 mwakani. Nchi hiyo ina viwanja viwili pekee vikubwa ambapo mmoja uko katika mji kuu wa Malabo na mwingine katika mji wa Bata. Haijawekwa wazi kama wenyeji hao wapya wataweza kushiriki michuano hiyo hiyo kwani waliondolewa katika hatua za awali kwa kosa la udanganyifu.
No comments:
Post a Comment