KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Shawky Gharib amewatema wachezaji wa Zamalek Ahmed El Shenawy, Hazem Emam na Ibrahim Salah katika kikosi chake kinachokabiliwa na mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Tunisia kutokana na majeruhi. Kocha amemuita golikipa mkongwe Essam El Hadary katika kikosi hicho baada ya kumuacha katika mchezo uliopita kwa madai kuwa golikipa huyo alikataa kuchezeshwa kama mchezaji wa akiba. Nyota hao walioachwa walipata majeruhi katika mchezo wa kufuzu michuano hiyo waliofungwa bao 1-0 Jumamosi iliyopita. Gharib amesema wameamua kumuita El Hadary kwa ajili ya mchezo huo wa mwisho kwakuwa anafanya vyema katika klabu yake ya Ismaily na ana uzoefu wanaohitaji lakini hataziba nafasi za majeruhi Emam na Salah. Kikosi kamili cha Misri kilitua jijini Tunis jana mchana tayari kwa ajili ya mchezo wao huo utakaochezwa Jumatano.
No comments:
Post a Comment