Monday, November 17, 2014

RAIS WA ZAMANI WA BARCELONA AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO CHAKE JELA.

RAIS wa zamani wa klabu ya Barcelona, Jose Nunez ameanza kutumikia kifungo chake rasmi jela jana baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kuhonga maofisa wa kodi. Vyombo vya habari nchini Hispania vilionyesha gari lililombeba Nunez likiwasili katika jela ya Quatre Camins iliyopo karibu na jiji la Barcelona ambako atatumikia kifungo cha miaka miwili na miezi miwili. Novemba 6 mwaka huu jaji alimpa Nunez mwenye umri wa miaka 83 muda wa siku 10 awe ameanza hukumu yake baada ya kushindwa rufani yake ya mwisho. Nunez alikutwa na hati ya kutoa hongo kwa maofisa wa kodi na mahakama mwaka 2011, kesi ambayo haikuhusisha klabu ya Barcelona. Nunez ambaye ni mmiliki wa kampuni ya ujenzi alikuwa rais wa Barcelona kuanzia mwaka 1978 mpaka mwaka 2000.

No comments:

Post a Comment