RIPOTI ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, kuhusu tuhuma za rushwa katika nchi zilizokuwa zikiwania nafasi ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2011 imedaiwa kuwa na dosari. Anayehoji kuhusu ripoti hiyo ni wakili Michael Garcia ambaye alifanya uchunguzi kwa kipindi cha miaka miwili kuhusu tuhuma hizo za rushwa. Ripoti ya FIFA yenye kurasa 42 ilizisafisha nchi za Urusi na Qatar ambazo zitakuwa wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022. Lakini ilituhumu Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kwenda kinyume na utaratibu wa kutaka nafasi ya kuandaa michuano ya 2018 na kuiharibia FIFA sifa. Garcia ambaye ni mwanasheria kutoka Marekani aliyepewa jukumu hilo la uchunguzi amedai kuwa ripoti hiyo imefurugwa.
No comments:
Post a Comment