Monday, November 17, 2014

DEL BOSQUE AKANUSHA KUWATISHIA COSTA NA FABREGAS.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amekanusha kuwatishia wachezaji majeruhi Diego Costa na Cesc Fabregas kwa kusema itakuwa ngumu kwao kurejea katika kikosi chake. Beki Sergio Ramos alizua mjadala wiki iliyopita wakati alipotoa kauli kuhusiana na kujituma kwa wachezaji katika timu ya taifa kauli ambayo ilichukuliwa kama kijembe kwa Costa na Fabrigas. Nyota hao wawili wa Chelsea hawakuwepo katika kikosi cha Hispania kilichocheza mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 na Belarus Jumamosi iliyopita huku wakitarajiwa pia kutokuwepo katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ujerumani kesho. Kufuatia ushindi wa mabao 3-0 waliopata Hispania katika mchezo wa Jumamosi, Del Bosque amesema haitaweza kuwa rahisi kwa Costa na Fabregas kurejea moja kwa moja katika kikosi chake wakati watakapokuwa fiti. Lakini alirekebisha kauli yake hiyo kwa kufafanua kuwa kuna ushindani mkubwa katika kikosi chake hivi sasa kutokana na vijana wanaochipukia ndio maana akasema hivyo.

No comments:

Post a Comment