NAHODHA wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amedai kuwa wachezaji wenzake wanapaswa kujirejeshea hali ya kujiamini kama wanataka kurejesha nyakati za furaha katika Uwanja wa Emirates. Kabla ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa, Arsenal walikubali sare ya mabao 3-3 dhidi ya Anderlecht katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kuongoza wao kwa mabao matatu kabla ya kuja kufungwa na mabao 2-1 na Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu. Akihojiwa Arteta amesema wachezaji wenzake wnapaswa kusahau yaliyowatokea nyuma na kuhakikisha hawarudii tena makosa ya kupoteza mchezo wakati tayari wakiwa wanaongoza. Arteta aliendelea kudai kuwa kwasasa hawapaswi kuweka nyuso za huzuni kwani yaliyopita yamepita na wanapaswa kuhakikisha wanaamsha morali ili wafanye vyema. Arsenal kwasasa wako katika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 17 katika mechi 11 walizocheza mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment