Monday, November 17, 2014

KENYA, SUDAN, ZIMBABWE ZATUPWA NJE KINYANG'ANYIRO CHA UENYEJI WA AFCON 2017.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limetangaza majina ya nchi nne zitakazokuwepo katika kinyang’anyiro cha kugombea uenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwaka 2017. Katika kikao chake walichokutana wiki iliyopita CAF imezitaja nchi za Algeria, Gabon, Misri na Ghana kuwa nchi zilizoteuliwa katika kinyang’anyiro hicho huku nchi za Kenya, Sudan na Zimbabwe zikiondolewa kwa kukosa kutimiza vigezo vilivyohitajika. CAF inatafuta nchi mbadala itakayochukua nafasi ya Libya ambao walijiondoa kutokana na suala la usalama na uamuzi wa mwenyeji mpya unatarajiwa kutoklewa mapema mwakani. Soka la Misri limekuwa likisuasua toka kuondolewa kwa utawala wa zamani wa rais Hosni Mubarak mwaka 2011 na kupelekea kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha soka kusimama kwa baadhi ya vipindi kutokana na vurugu. Hata hivyo Misri ndio nchi yenye mafanikio zaidi kwa kunyakuwa taji la Afcon mara saba ingawa walishindwa kufuzu katika michuano hiyo mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment