Monday, November 17, 2014

MWENYEKITI WA ZAMANI WA FA ATAKA MATAIFA YA ULAYA KUUNGANA NA KUGOMEA KOMBE LA DUNIA 2018.

MWENYEKITI wa zamani wa Chama cha Soka Uingereza-FA David Bernstein amekikata chama hicho kulishawishi Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kuratibu mgomo wa nchi za bara hilo kushiriki Kombe la Dunia mpaka Shirikisho la soka Duniani-FIFA litakapojifanyia marekebisho. Bernstein ambaye alikuwa mwenyekiti wa FA kati ya mwaka 2011 na 2013, ndiye ofisa mwingine wa juu kutaka mataifa ya Ulaya kuungana na kuchukua hatua kufuatia taarifa za kukanganya zilizotolewa na FIF kuhusu zabuni ya kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022. Akihojiwa Bernstein pia amekosoa uamuzi wa FIFA kuwa wa kimabavu kwa kuichagua Qatar kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Bernstein amesema baada ya kutoka kwa ripoti ambayo imekosolewa na aliyehusika kufanya uchunguzi anadhani wakati umefika sasa kuiwajibisha FIFA kabla ya hawajadidimiza kabisa mchezo wa soka. Kiongozi huyo aliendelea kudai kuwa FA pekee hawajaweza kufanikiwa katika vita hivyo ndio maana anadhani wakiungana na UEFA watawez kufanikiwa kwani Kombe la Dunia bila timu za Ulaya litakuwa halina mvuto.

No comments:

Post a Comment