Wednesday, November 5, 2014

EBOLA YAIHENYESHA CAF.

PAMOJA na kutaa ombi la kuahirisha michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani, Shirikisho la Soka barani Afrika bado lina hofu na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. CAF imeipa Morocco mpaka Jumamosi hii kutoa uamuzi wao kama wataanza michuano hiyo au wataahirisha. Morocco imeonyesha hofu ya kuandaa michuano hiyo kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za Afrika ya Magharibi. Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani amesema hali sio nzuri kwao wote kwani hata wao wana hofu. Amrani amesema wanaelewa tahadhari ambayo taifa huru kama Morocco lina haki ya kuchukua lakini jambo muhimu hapo ni kutoongeza hofu badala yake ni kuwa wazi kuhusu vile unavyoweza kuambukizwa kutoka eneo moja kwenda jingine huku wakichukua tahadhari. Amrani ameongeza kuwa CAF imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Shirika la Afya Duniani-WHO ili kuhakikisha hakuna hatari zozote

No comments:

Post a Comment