POLISI wa mji wa Dortmund wamedai kuwa shabiki yeyote wa soka aliyehusika katika vurugu wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Borussia Dortmund na Galatasaray atapewa adhabu anayostahili. Maofisa wawili wa polisi walijeruhiwa, huku watu 21 wakikamatwa na baadhi ya mashabiki 700 wa Uturuki wakifanyiwa uchunguzi wa tabia zao baada ya kuzuka vurugu katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa jana. Klabu ya Borussia Dortmund waliokuwa wenyeji wa mchezo huo wamesisitiza kuwa waliweka usalama wa kutosha kuhakikisha mashabiki wakorofi hawahudhurii mchezo huo lakini baadae baadhi yao walionekana uwanjani. Zaidi ya viti 20 viliharibiwa na mashabiki wa Galatasaray wakati wa vurugu hizo ambapo itaigharimu Dortmund kiasi cha euro 30,000 kuweka vingine. Galatasaray ambao kwasasa wanashika mkia katika kundi lao wanaweza kukabiliwa na adhabu wakati Shirikisho la Soka la Ulaya litakapofanya uchunguzi wake.
No comments:
Post a Comment