Thursday, November 13, 2014

KAULI YA KIBAGUZI YAMPONZA KOCHA URUSI.

SHIRIKISHO la Soka la Urusi limedai kumsimamisha kocha klabu ya Rostov, Igor Gamula kwa muda wiki tano bada ya kupatikana na hatia ya kutoa maoni ya kibaguzi. Gamula aliadhibiwa baada ya kuwaambia waandishi wa habari kuwa klabu yake inawachezaji weusi wa kutosha hivyo hana haja ya kusajili wengine zaidi. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 ameomba radhi kwa kila mmoja wa wachezaji hao kutokana na kauli yake hiyo. Hata hivyo, amesisitiza kuwa kauli yake hiyo ilikuwa kwa utani zaidi kwani amekuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wa Afrika lakini anadhani vyombo vya habari vya Uingereza havikuelewa utani wao Warusi.

No comments:

Post a Comment